70 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Anas, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Bakr bin Muhammad bin ´Amr bin Hazm, kutoka baba yake, kutoka kwa ´Amr bin Sulaym az-Zarqiy, Abu Humayd as-Saa´idiy amenikhabarisha ya kuwa walisema:

”Ee Mtume wa Allaah! Tunakuswalia vipi?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد و أزواجه و ذريته، كما صليت على آل إبراهيم، و بارك على محمد و أزواجه و ذريته، كما باركت على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na wakeze na kizazi chake kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Na mbariki Muhammad na wakeze na kizazi chake kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Abu Daawuud ameipokea kwa cheni ya wapokezi ya mtunzi. Ameipokea tena yeye, al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kupitia njia zingine kutoka kwa Maalik. Ipo katika “al-Muwattwa’” (1/165/666).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 66
  • Imechapishwa: 31/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy