71. Hadiyth ”Umetuamrisha kukutakia amani… ”

71 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Ayyuub, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Bishr bin Mas´uud, ambaye ameeleza:

”Kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah! Umetuamrisha kukutakia amani na kukuswalia. Tumejua namna ya kukutakia amani, tunakuswalia vipi?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على آل محمد، كما صليت على آل إبراهيم، و بارك على آل محمد، كما باركت على آل إبراهيم

“Ee Allaah! Wasifu jamaa zake Muhammad kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Na wabariki jamaa zake Muhammad kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. Wanamme wote ni wanamme wa Muslim. ´Abdur-Rahmaan bin Bishr bin Mas´uud alikuwa ni Abu Bishr al-Answaariy al-Madaniy al-Azraq. Amepokea kutoka kwa Abu Mas´uud al-Answaariy, Abu Hurayrah, Abu Sa´iyd na Khabbaab al-Arat. Ibn Hibbaan amemtaja katika “ath-Thiqaat” ilihali ad-Daraqutwniy yeye amesema kwamba ”amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na Swahabah katika cheni ya wapokezi”. Kana kwamba anaashiria Hadiyth yake hii.  Imepokelewa kwa cheni ya wapokezi iliyoungana kupitia kwa Abu Mas´uud al-Answaariy, lakini sio Swahiyh, kama itakavyoonekana katika ukaguzi unaofuata.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 67
  • Imechapishwa: 31/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy