72. Hadiyth ”Hakika tumejua namna ya kukutakia amani… ”

72 – Musaddad ametuhadithia: Yaziyd bin Zuray´ ametuhadithia: Ibn ´Awn ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Bishr bin Mas´uud, ambaye amesema:

”Walisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika tumejua namna ya kukutakia amani, tunakuswalia namna gani?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد، كما صليت على آل إبراهيم، اللهم بارك على محمد، كما باركت على آل إبراهيم

“Ee Allaah! Msifu Muhammad kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Ee Allaah! Mbariki Muhammad kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. Imeshazungumziwa katika Hadiyth iliyotangulia.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 67-68
  • Imechapishwa: 31/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy