Swali: Ni upi usahihi wa mahala pa kaburi la Nabii Yuunus (´alayhis-Salaam) ni ´Iraaq?

Jibu: Ama Yuunus (´alayhis-Salaam) haijulikani kaburi lake na wala hili halina usahihi. Bali makaburi ya Mitume wote hayajulikani, ila tu kaburi ya Mtume wetu Muhammad (´alayhis-Salaam) inajulikana, alizikwa nyumbani kwake Madiynah (´alayhis-Salaam). Hali kadhalika kaburi la Mtume Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alizikwa Palestina. Ama wasiokuwa hao wawili, wamebainisha wanachuoni ya kwamba hayajulikani makaburi yao. Na mwenye kudai ya kwamba hii ni kaburi ya fulani au fulani, ni muongo. Halina asli wala usahihi. Na mwenye kusema kaburi la Yuunus liko mahali fulani, halina asli. Inatakikana lijulikane hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 31/01/2024