Kwanini Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab inaonekana kuwa maalum?

Kubwa walo nalo, ni kuwa Shaykh alisimama kwa jambo hili (mwenyewe) akasubiri na kustahamili. Na wanachuoni wenzake walinyamaa na kubaki katika raha. Wanaweza kutumia hoja hii na kusema, kwa nini Shaykh alikuwa katika zama za wanachuoni, kwa nini yeye mwenyewe tu ajishughulishe na jambo hili [la kulingania katika Tawhiyd]? Tunasema kuwa hii ni fadhila ya Allaah anampa amtakae. Ni kweli kwamba kuna wanachuoni wengi Najd, lakini hawakusimama kwa jambo hili, bali walibaki katika raha. Walichokuwa wanakipa umuhimu ni vitabu vya Fiqh na wala hawakuipa umuhimu ´Aqiydah wala Tawhiyd. Hivyo, Allaah akawa amewaharamishia hilo. Na Allaah akamneemesha Shaykh na kusimama imara. Watu hawa, pengine walikuwa hawana subira na ustahamilivu. Sisemi kuwa wote wanapenda upotofu, lakini ninachosema ni kuwa, wengine wao yawezekana walikuwa hawana subira wala ustahamilivu. Au walikuwa na ukataji tamaa, baadhi yao wana ukataji tamaa na kuona kuwa haina manufaa, hatuwezi kuwashinda watu hawa na kadhalika. Shaykh (Rahimahu Allaah) Allaah alimpa nguvu ya Imani na nguvu ya elimu na nguvu ya hoja. Akastahamili maudhi na akasubiri na akasimama kwa jambo hili. Na fadhila zake kwa nchi hii na kwa nchi za waislamu hazikatawi, naye ana ujira mfano wa ujira wa mwenye kumfuata mpaka siku ya Qiyaamah. Kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayelingania katika uongofu, ana ujira mfano wa ujira wa atakayemfuata, hakutopungua lolote katika ujira wake. Na atakayelingania katika upotofu, juu yake ana madhambi mfano wa madhambi wa atakayemfuata, hakutopungua lolote katika madhambi yake.”

Na fadhila za Allaah anampa amtakae. Na Allaah hutuma katika Ummah huu – kutokana na fadhila Zake – katika kila karne mtu ambaye anasimama kwa dini hii na kuilingania. Kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Halitoacha pote katika Ummah wangu kuwa juu ya haki wazi wazi… ” Anasema (Ta´ala):

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ

“Na Tukawajaalia miongoni mwao maimamu wanaongoza kwa amri Yetu waliposubiri; na walikuwa ni wakiziyakinisha Aayah Zetu.” (32:24)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=ARoBk8JGNLk
  • Imechapishwa: 31/01/2024