Mke amtolee Zakaat-ul-Fitwr mke kukiwa kuna ugomvi kati yao?

Swali: Je, mume analazimika kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mke ambaye kati yao kuna magomvi makubwa?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr inamlazimu mtu mwenyewe na kila ambaye analazimika kumhudumia akiwemo mke kwa sababu ni lazima kumpa matumizi. Kukiwa kati yao kuna mgogoro mkubwa ambao hukumu yake imepelekea kuwa ni muasi na kuanguka kumhudumia, basi haitomlazimu kumtolea Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu ni yenye kufuatia matumizi yake na hivyo Zakaat-ul-Fitwr inadondoka kwa kudondoka kwake matumizi.

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdul-´Aziyz bin Maaniy´

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/368) nr. (606)
  • Imechapishwa: 10/05/2022