Zakaat-ul-Fitwr kwa yatima ninayemfadhili nje ya nchi?

Swali: Je, nimtolee Zakaat-ul-Fitwr yatima ambaye ninamfadhili huko Afrika?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr mtu anaitoa katika ile nchi ambayo Ramadhaan imemkuta akiwa ndani yake. Kwa sababu ni yenye kufuata mwili. Yatima mkusudiwa atajitolea mwenyewe katika nchi yake au atatolewa na jumuiya inayosimamia suala la kumwangalia huko alipo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (08/265) nr. (17299)
  • Imechapishwa: 10/05/2022