Swali: Mwanaume amemuoa mwanamke na baada ya kuchanganyika naye akaona kuwa amechanja. Je, hiyo inazingatiwa kuwa ni katika kasoro zinazohalalisha kuifuta ndoa?
Jibu: Hapana, sio kasoro. Hata hivyo kuchanja ni haramu kwake. Anatakiwa kuiondosha kwa njia yoyote. Lakini hata hivyo hiyo sio kasoro inayomhalalisha kuivunja ndoa.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
- Imechapishwa: 23/07/2023