Makabila yameamua mahari fulani

Swali: Baadhi ya makabila yamewekeana kikomo cha mahari kati yao na wakakubaliana juu ya kikomo hicho. Je, ni lazima kufanyia kazi kiwango hicho kwa njia ya Shari´ah?

Jibu: Hapana, sio lazima kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا

“Na mkitaka kubadlisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao [zawadi ya] mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote.”[1]

Mahari hayana kikomo na hivyo haitakiwi kuyawekea kikomo.

[1] 04:20

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 23/07/2023