Swali: Je, inafaa kuswali swalah ya Witr juu ya mnyama katika hali ya ukazi?

Jibu: Hapana. Hili linakuwa safarini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anaswali swalah iliyopendekezwa katika hali ya ukazi. Bali atatakiwa kushuka kutoka katika kipando chake na kuswali katika msikiti au nyumba. Kuhusu safari ni ndefu. Inaweza kuwa masaa marefu ambayo anayalipa msafiri juu ya kipando chake au juu ya gari yake. Hivyo anahitajia kuswali. Ama katika hali ya uenyeji mara nyingi masafa hayawi marefu. Inakuwa ni muda wa robo saa au nusu saa. Kisha baada ya hapo anarejea na kuswali katika nyumba, msikiti au maeneo mengine yoyote. Swalah ni nyepesi katika hali ya ukazi. Haikusuniwa kwa mtu kuswali juu ya mnyama au juu ya gari katika hali ya ukazi. Hili linakuwa katika hali ya safari.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 07/11/2021