Mjinga ametembea Sa´y mizunguko kumi na nne


Swali: Kuna mtu alifanya ´Umrah na wakati wa Sa´y akazunguka mizunguko kumi na nne kwa sababu ya kufahamu kwake vibaya. Je, ´Umrah yake ni yenye kukubaliwa na sahihi?

Jibu: ´Umrah yake ni yenye kukubaliwa. Mizunguko yake kumi na nne ni yenye kukubaliwa; saba ndio inayosihi na mingine saba ni ziada isiyokuwa na maana yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (106) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoul%20lahfan-%2027-03-1441.mp3
  • Imechapishwa: 16/09/2020