Wanawake kuswali mbele ya safu ya imamu

Swali: Je, inajuzu kwa wanawake kuswali mbele ya safu ambayo imamu anaswali ikiwa msikiti umejaa na hawawezi kuswali sehemu ya wanawake, wanaswali nje ya msikiti na wakifanya hivyo itakuwa safu yao mbele ya imaamu.

Jibu: Hili ni kosa wala haifai. Ima wawe nyuma ya wanawake au waswali majumbani mwao. Pia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza na kwamba bora ya swalah ya mwanamke ni katika nyumba yake.

Check Also

Mwanamke kuswali na Niqaab

Swali: Bora kwa mwanamke ni kuswali hali ya kuwa amefunua uso wake au ameufunika wakati …