Khawaarij, Mu´tazilah na jopo kubwa katika Ashaa´irah wanaonelea kufaa kuwafanyia uasi watawala ambao ni wanyanyasaji na watenda madhambi.

Kuhusu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini kuwa midhali mtawala bado ni muislamu basi ni wajibu kumtii katika mema na haijuzu kumfanyia uasi. Hii ni sifa inayowapambanua Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wengine. Bali maimamu wa Ahl-ul-Hadiyth katika zama za fitina mwishoni mwa karne ya tatu na ya nne walikuwa wakiwajaribu watu kwa suala hili kama wanaonelea kuwa inafaa kuwatii [viongozi] au haifai. Uhakika wa mambo ni kwamba kuna maimamu ambao wamesema:

“Alama ya Ahl-us-Sunnah ni kuwaombea du´aa wafalme. Na alama ya Ahl-ul-Bid´ah ni kuwatukana wafalme.”

Hili ni jambo liko wazi kwa yule ambaye anatambua mwongozo na misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Miongoni mwa waliotaja haya ni pamoja vilevile na Ibn Battwah katika “al-Ibaanah” na al-Barbahaariy katika “Sharh-us-Sunnah”. Huyu ni miongoni mwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambaye amefafanua hilo vya kutosha. Hili ni kutokana na yaliyotokea katika zama zake kwa sababu ya kuwepo kwa wengi wenye kwenda kinyume na msingi huu mkubwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 149-150
  • Imechapishwa: 27/08/2020