Mjane kwenda kufanya ´Umrah au Hijjah ndani ya eda

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke aliye ndani ya eda ya kufiwa na mume wake kutoka kwenda kufanya ´Umrah?

Jibu: Hapana. Asitoke kwa ajili ya kufanya ´Umrah wala Hajj mpaka imalizike eda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu mwanamke aliyefiwa na mume wake:

“Baki nyumbani mpaka eda imalizike.”

Lakini ikiwa mume atakufa ilihali mwanamke huyu yuko njiani? Wamesema ikiwa ameshafika ule umbali unaoruhusu kufupisha swalah, basi ataendelea katika ´Umrah au Hajj yake. Ikiwa ni chini na yale masafa yanayoruhusu kufupisha, basi anatakiwa kurejea katika nyumba yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 10/04/2023