Mjamzito na mnyonyeshaji katika Ramadhaan

Swali: Ni lini inaruhusu kuacha kufunga kwa mjamzito na myonyeshaji katika Ramadhaan? Ni vitu gani vinavyoharibu swawm kwa ujumla? Inajuzu kwa mwanamke kutumia dawa zinazozuia hedhi ili aweze kufunga Ramadhaan bila ya usumbufu?

Jibu: Inajuzu kwa mjamzito na mnyonyeshaji kula endapo watakhofia kwa watoto wao swawm kuwadhuru. Kwa sababu swawm inaweza kudhoofisha kile chakula ambacho mtoto hula tumboni mwa mama yake. Mambo yakiwa hivo basi inafaa kwao kuacha kufunga na walipe wakati mwingine pamoja na kulisha vilevile. Ikiwa watachelea juu ya nafsi zao kwa sababu hawawezi kufunga hali ya kuwa ni wajawazito na wanyonyeshaji, basi inafaa kwa wao kula na kulipa siku nyenginezo. Haiwalazimu kulisha. Haya ni kuhusu mjamzito na mnyonyeshaji.

Inajuzu vilevile kwa mwanamke kutumia dawa inayozuia hedhi ili aweze kufunga ikiwa dawa hii haidhuru afya yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 06/06/2017