Mitetemeko mingi ya ardhi na wanachuoni wachache

Swali: Ni jambo linalotambulika kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) peke yake ndiye mwenye kujua ni lini Qiyaamah kitatokea. Lakini hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametaja baadhi ya alama zake ikiwa ni pamoja na yale aliyosimulia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa Qiyaamah hakitotokea mpaka kwanza:

“… elimu ipotee, mitetemeko ya ardhi iwe mingi na fitina ziwe nyingi… “

Zipo alama nyenginezo zitazotokea kabla ya Qiyaamah. Mitetemeko ya ardhi iliokithiri hii leo ni miongoni mwa alama za Qiyaamah?

Jibu: Udhahiri ni kwamba mitetemeko mingi ya ardhi na fitina nyingi ni miongoni mwa alama za Qiyaamah. Fitina kama mnavyojionea wenyewe hii leo zimekuwa nyingi. Alama za Qiyaamah ni nyingi. Mitetemeko ya ardhi ni mingi. Wanachuoni wa haki pia ni wachache. Wanachuoni wengi hii leo ima malengo yao makubwa ni kuiridhisha dola au watu ni wachache mno ambao malengo yao ni kuitumikia dini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (9 B)
  • Imechapishwa: 13/08/2020