24- Madhambi yanapelekea maporomoko na mitetemeko ya ardhi

Miongoni mwa athari za kumuasi Allaah ardhini ni kwamba yanapelekea katika maporomoko, mitetemeko ya ardhi na kuondosha baraka yake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita Thamuud na akawakataza Maswahabah kuingia ndani ya miji yao isipokuwa hali ya kuwa wanalia. Mpaka akawakataza kunywa maji yao na kuwanywesha maji hayo vipando vya wanyama wao. Alifikia mpaka kuwakataza unga uliotengenezwa kwa maji hayo wasiwape ngamia. Yote haya ni kutokana na ile athari mbaya ya maasi kwenye maji. Kadhalika ile athari mbaya ya madhambi imeathiri kupunguka kwa matunda na maafa mengine unayoona. Imaam Ahmad ametaja katika “al-Musnad” yake:

“Kwenye ghala ya Banuu Umayyah kulikuweko nafaka ya ngano kubwa kiasi cha kokwa ya tende. Ilikuwa kwenye mkoba ambao umeandikwa juu yake “Hii ilichipuka katika zama za uadilifu.”

Mengi katika maafa haya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huyaleta pale ambapo waja wanaanza kufanya madhambi. Wengi katika wakuu wa majangwa wamenieleza namna ambavyo matunda yalikuwa makubwa zaidi hapo zamani na kwamba mengi katika majanga yanayotokea hii leo walikuwa si wenye kuyatambua.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 79
  • Imechapishwa: 13/08/2020