Mirathi ya watoto kutoka kwa babu ambao baba yao amefariki

Swali: Ni ipi hukumu ya watoto wa mwana aliyefariki kabla ya baba yake kuhusu urithi wa babu yao hali ya kuwa mwana aliyefariki ana ndugu wa kiume na wa kike?

Jibu: Hawana mirathi kutoka kwa babu yao. Ikiwa baba yao alikufa kabla ya babu yao, basi hawarithi. Mirathi inakuwa kwa ndugu wa baba yao. Lakini inapendekezwa kwa babu yao kuwausia kitu katika theluthi au chini yake ili kuwafariji kutokana na msiba wao wa kufiwa na baba yao. Hivyo inapendekezwa awaandikie wasia wa theluthi yake, robo yake, sehemu ndogo kama tano au kiasi fulani cha mali, kwa kuwa wao si warithi. Kadhalika inapendekezwa kwa ami zao kuwasaidia ikiwa baba yao hakuwasia. Lakini si wajibu kama wanavyodhani baadhi ya watu. Hapana, si wajibu. Bali ni msaada tu.

Swali: Huyu mwana aliyekufa huenda alikuwa pia sababu ya mali iliyopo sasa, kwa nini watoto wake wananyimwa?

Jibu: Haijalishi kitu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wewe na mali yako ni milki ya baba yako.”

Ikiwa hakuwa na mali maalum iliyotengwa na wala baba yake hakumpa kitu maalum, bali mali iko kwa jina la baba, basi mali ni ya baba.

Swali: Baadhi ya watu wanasema babu ana haki ya kuwaweka wao mahali pa baba yao?

Jibu: Hakuna ubaya. Ikiwa atawausia, basi hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3408/حكم-توريث-ابناء-الابن-المتوفى-قبل-والده-من-ميراث-الوالد
  • Imechapishwa: 07/09/2026