Swali: Mama yangu mara nyingi huniomba kumpeleka safari mbalimbali za huku na kule na tunakusanyika zote nyumbani kwake kila siku, jambo ambalo halifichikani kwako kwamba ndani yake kuna kupoteza muda na umri pasi na faida. Mimi ninahisi uzito juu ya kumtii. Haya ninayofanya hivi sasa yananipotezea muda. Nikipunguza kumtembelea na kutoka naye nakuwa nimemuasi. Nahisi kuchanganyikiwa na naomba maelekezo.

Jibu: Ikiwa hupatwi na madhara kwa kule kumuitikia basi muitikie. Ikiwa unapatwa na madhara au unapitwa na manufaa, basi usimuitikie isipokuwa kwa dharurah. Safari za hapa na pale, kuwatembelea ndugu na marafiki sio jambo la dharurah. Ikiwa kule kumuitikia maombi yake kunakufanya kupitwa na manufaa au kunakutumbukiza katika madhara, basi hapo si wajibu kumuitikia. Lakini ni lazima kwako kumshawishi na kumkinaisha. Ama ikiwa jambo hilo halina madhara kwako au yeye ndiye atapatwa na madhara zaidi iwapo utakataa kumuitikia, basi muitikie. Hapa kunavuliwa kumkubalia au kumuitikia na wakati huohuo kukakufanya kuacha jambo la wajibu. Katika hali hii itakuwa haijuzu. Ni kama mfano kumuitikia kukawa kunakushughulisha kutokamana na kusimamisha swalah ya mkusanyiko. Katika hali hii hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1009
  • Imechapishwa: 19/01/2019