Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
140 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
إنَّ اللهَ لَيَرْضَى عَنِ العَبْدِ أنْ يَأكُلَ الأَكْلَةَ، فَيَحمَدَهُ عَلَيْهَا، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ، فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا
“Hakika Allaah anaridhia kwa mja anapokula mlo akamshukuru kwa mlo huo na anapokunywa kinywaji akamshukuru kwa kinywaji hicho.”[1]
Katika Hadiyth hii kuna dalili inayoonyesha kuwa radhi za Allaah (´Azza wa Jall) zinaweza kupatikana kwa sababu ndogo kabisa. Radhi Zake zinaweza kupatikana kwa sababu hii. Allaah anaridhia pale ambapo mtu anapomaliza kula aseme “Alhamdulillaah” na anapomaliza kunywa aseme “Alhamdulillaah.”Kula na kunywa kuna adabu zake za kimatendo na za kimaneno.
1 – Adabu za kimatendo moja wapo ni kula kwa mkono wa kulia na kunywa kwa mkono wa kulia. Si halali kwake kula au kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto. Hili ni haramu kwa maoni yaliyo na nguvu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu kula au kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto na akaeleza kuwa shaytwaan anakula na kunywa kwa mkono wake wa kushoto. Kuna mtu alikula pamoja naye kwa mkono wa kushoto, akamwambia:
“Kula kwa mkono wako wa kushoto.” Yule mtu akasema: “Siwezi.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Na hutoweza.”
Baada ya hapo yule mtu hakuweza kunyanyua mkono wake wa kulia kwenda mdomoni mwake[2]. Hii ni adhabu alipewa.
2 – Adabu za kimaneno moja wapo ni kuleta Tasmiyah kabla ya kula. Aseme “Bismillaah”. Sahihi ni kwamba Tasmiyah wakati wa kula au kunywa ni wajibu na kwamba mtu anapata dhambi ikiwa hakumtaja Allaah katika kula au kunywa kwake. Kwa sababu ikiwa hakumtaja Allaah wakati wa kula na kunywa, shaytwaan anakula na kunywa pamoja naye.Hivyo basi, ni wajibu kwa mtu anapotaka kula amtaje Allaah. Endapo kabla ya kuanza kula atasahau kutaja jina la Allaah na akakumbuka katikati ya chakula, badala yake aseme:
بِسْمِ اللَّهِ فِي أَوَّلِهِ وَآخِرِهِ
“Kwa jina la Allaah, mwanzo na mwisho wake.”
Mtu akisahau kumtaja Allaah mkumbushe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkumbusha ´Umar bin Abiy Salamah wakati aliposogea na kula akamwambia:
“Ee kijana! Mtaje Allaah, kula kwa mkono wako wa kulia na kula kilicho mbele yako.”[3]
Hapa kuna dalili juu ya kwamba ikiwa watu wako kikundi ni wajibu kwa kila mmoja alete Tasmiyah kivyake. Haitoshelezi kwa mtu mmoja akaleta Tasmiyah kwa niaba ya watu wote. Kila mmoja anatakiwa kuleta Tasmiyah yake.
Kuhusiana na adabu wakati wa kumaliza, amhimidi Allaah (´Azza wa Jall) kwa neema hii kwa kule Allaah kumsahilishia chakula hichi pamoja na kuwa hakuna yeyote awezaye kufanya ikawa sahali. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ
”Je, mnaona maji ambayo mnakunywa? Je, ni nyinyi ndio mliyoyateremsha mawinguni au Sisi ndio wateremshaji?”[4]
[1] Muslim
[2]Muslim (2021).
[3]al-Bukhaariy (5376) na Muslim (2022).
[4] 56:68-69
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/204-205)
- Imechapishwa: 22/09/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/204-205)
Imechapishwa: 22/09/2024
https://firqatunnajia.com/miongoni-mwa-adabu-za-kula-na-kunywa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)