Miji ya Kiislamu pasina kuwa na Uislamu, miji ya makafiri na Uislamu

Swali: Baadhi ya walinganizi wanasema kuwa wametembelea miji ya Kiislamu na kuona kuwa kuna waislamu pasina kuwa na Uislamu na wametembelea miji ya magharibini na kuona kuwa wana Uislamu pasi na kuwa na waislamu. Je, maneno haya ni kusifu yale waliyonayo? Je, inajuzu kwa mtu kusema namna hii?

Jibu: Maneno kama haya hayajuzu. Mtu wa kwanza maneno haya kujinasibisha nayo ilikuwa ni Muhammad ´Abduh ambaye alikuwa ni muftiy wa Misri katika wakati wake. Yeye ndiye aliyejinasibisha na maneno haya.

Vovyote waislamu watakavokuwa na vovyote wadhaifu walivo ni bora kuliko makafiri. Hata Muislamu alopetuka kwa kutenda madhambi na mwasi ni bora kuliko kafiri. Kafiri asifadhilishwe kamwe juu ya muislamu. Hili halijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa