Ummah wa Kiislamu ni kundi moja. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ

“Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, hivyo basi niabuduni.” (21:92)

Njia na mfumo wake ni mmoja. Amesema (Ta´ala):

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni na wala msifuate njia za njia za vichochoro zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na taqwa.” (06:153)

Tunaona leo kuna makundi na mapote mengi. Kila kundi limejiwekea njia na kujifanyia mfumo likilingania katika mfumo huo. Sambamba na hilo utakuta makundi na mapote haya yamefarikiana na ni yenye magomvi na mizozo na yale makundi na mapote yaliyokutwa. Makundi na mapote haya yanapenda na kuchukia kwa ajili ya mifumo hii waliyowekewa na viongozi wao na yanawalazimisha wafuasi wasitoke nje ya mifumo yake. Endapo atafanya hivo basi atasuswa. Hachukui na hapewi isipokuwa ikiwa atafuata ile mipaka aliyowekewa na chini ya zile nembo zake. Viongozi wa makundi na mapote haya wanaonelea kuwa Uislamu na mafunzo yake yote yamekomeka katika mfumo huu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bid´ah – Dhwawaabitwuhaa wa atharuhaa as-Sayyiu´ fiyl-Ummah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 27/08/2020