Tumetangulia kutaja maana ya Bid´ah na kwamba ni yule anayezua Bid´ah akalingania kwayo na akajenga uadui kwa ajili yake. Vilevile tumetangulia kusema kuwa Bid´ah imegawanyika sehemu mbili; Bid´ah inayomfanya mtu kuwa kafiri na Bid´ah isiyomfanya mtu kuwa kafiri na tumetaja maneno ya wanachuoni kuhusu yule mwenye kuifanya.

Kuhusiana na mwenye kutekeleza katika baadhi ya mambo na wakati huohuo akawa ni mwenye kujulikana katika mfumo na tabia yenye kusifiwa na kuwa na elimu ya Kishari´ah, kosa lake halishushi hadhi yake. Akiwa bado yuko hai basi ni lazima kumzindua juu ya kosa lake kwa njia iliokuwa nzuri yenye kujulikana kati ya wanachuoni. Nasaha hii iwe imejengwa juu ya kusaidiana katika wema na uchaji Allaah. Kwa sababu dini ni kupeana nasaha. Kinachotakiwa ni kumpa nasaha mwanafunzi huyu kutegemea na nafasi yake. Mtu anatakiwa kufanya hivo kwa adabu na heshima na vilevile kumbainishia haki kwa dalili pasi na ukali na kumpandia juu. Inatakiwa iwe kwa hekima na maneno yaliokuwa mazuri ili malengo yaweze kufikiwa. Lengo ni ili umoja na mapenzi kwa ajili ya Allaah yaweze kubaki. Hakika si vyengine, waumini ni ndugu.

Ama ikiwa mtelezaji huyu ameshatangulia mbele ya Mola Wake basi anatakiwa kuombewa du´aa. Mitume peke yao ndio waliokingwa na kukosea. Kinachotakiwa ni kuwabainishia watu makosa ya watu hawa ili watu wasije kuwafuata katika makosa hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bid´ah – Dhwawaabitwuhaa wa atharuhaa as-Sayyiu´ fiyl-Ummah, uk. 27
  • Imechapishwa: 27/08/2020