Midhali umemuuliza mwanachuoni basi hakuna dhambi juu yako

Swali: Mwanamume kabla ya miaka kumi ya nyuma alimwamrisha mke wake ambaye ananyonyesha kutofunga katika mchana wa Ramadhaan kwa sababu ya kunyonyesha na akamwambia kwamba hakuna kinachomlazimu isipokuwa kulisha peke yake na kwamba yeye ndiye atamtolea chakula. Mume wake alimwambia kwamba amepewa fatwa hiyo na wanachuoni. Katika mwaka huu tuliomo nimepata kujua kwamba analazimika kulipa na kulisha. Ni yepi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Maoni yangu juu ya hilo ni kwamba hakuna kinchomlazimu. Midhali mume wake amepewa fatwa hiyo na baadhi ya wanachuoni na wakamwambia kwamba hakuna kinachomlazimu isipokuwa tu kulisha, basi hakuna kinachomlazimu. Lakini maoni sahihi ni kwamba ni lazima kwake kulipa kutokana na kuenea kwa maneno Yake (Ta´ala):

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Kuhusu yaliyopita ambayo yalijengeka juu ya fatwa aliyomnukulia mumewe, hakuna kinachomlazimu. Vivyo hivyo kila masuala ambayo ambaye si msomi atamuuliza yule ambaye anaamini kuwa ni msomi kisha akafutiwa kinyume na usawa, hakuna kitu kitachomlazimu. Lakini kwa sharti ajue kuwa huyu anayemuuliza anastahiki kweli kufutu. Si kila mwenye kuvaa kilemba na akaachia ndevu anakuwa mwanachuoni. Kuna uwezekano akawa ni mjinga. Lakini akijua kwa vile mtu huyo ni maarufu, watu wanamuuliza na kwamba anastahiki kuombwa fatwa ambapo akamjibu lakini ikaenda kinyume na usawa, basi yule muulizaji hana dhambi yoyote.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1506
  • Imechapishwa: 13/06/2020