Kununua mazawadi baada ya Twawaaf-ul-Wadaa’

Swali: Baadhi ya watu wanapomaliza Twawaaf-ul-Wadaa’ wanaenda kununua mazawadi kwa ajili ya ndugu na marafiki zao…

Jibu: Mambo ya safari hayana neno hata kama watu watanunua baada ya Twawaaf-ul-Wadaa’. Vivyo hivyo ikiwa mtu atanunua chakula au mahitajio mengine ya safari. Hakuna neno. Hata hivyo Twawaaf-ul-Wadaa’ itatakiwa kurejelewa ikiwa mtu atanunua kitu kwa ajili ya biashara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 13/06/2020