Michezo ya mieleka, mashindano ya magari na ndege

Swali: Je, kupanda baharini kunaweza kulinganishwa na kuharamisha baadhi ya michezo kama mieleka?

Jibu: Mieleka inayojumuisha kupigana kupiga ni haramu. Lakini mieleka ya kawaida, yaani ile ambayo mtu anajaribu kumwangusha mwenzake bila madhara haina tatizo. Hata hivyo mieleka ambayo mtu anapiga mwenzake kwenye mgongo, kichwa au sehemu nyingine, haijuzu. Ni khatari.

Swali: Vipi kuhusu mashindano ya magari?

Jibu: Mashindano ya kukimbia kwa miguu, kwa farasi na kwa ngamia hayana tatizo, kwa sababu Sunnah imekuja kuyasapoti. Lakini mashindano ya magari hapana shaka kwamba ni khatari. Maoni yanayosema kuwa ni haramu ni yenye nguvu. Naona kuwa hakuna sababu ya kunifanya kuruhusu mashindano ya magari au ndege. Maoni yanayosema kuwa ni haramu yana nguvu, kwani yana khatari kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24929/حكم-المصارعة-والمسابقة-بالسيارات
  • Imechapishwa: 07/01/2025