31 – Hajjaaj bin Minhaal ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-Jabbaar amenikhabarisha: Nimemsikia Muhammad bin Ka´b, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Abu Hurayrah akisimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Kizazi ni tawi kutoka kwa Mwingi wa rehema. Kinasema: ”Ee Mola! Nimedhulumiwa! Nimekatwa! Ee Mola! Ee Mola! Ee Mola!” Ndipo Ajibu: ”Je, huridhi Nimkate yule mwenye kukukata na Nimuunge yule mwenye kukuunga?”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 12
  • Imechapishwa: 08/01/2025