Swali: Je, inaruhusiwa kwa imamu kama anataka kuswali Maghrib kwa kusoma al-A’raaf kuwatangazia waumini rasmi kwa karatasi kwamba leo atasoma Suurah hiyo?

Jibu: Dhahiri ni kwamba asisome na wala asitangaze, kwa sababu ni jambo la khiyari. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilifanya mara moja tu. Aidha amesisitiza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutorefusha. Watu wa zama hizi hawawezi kustahimili jambo hilo. Kwa maoni yangu naona kuwa haifai kusoma Suurah hiyo katika hali ya sasa, kwa sababu watu hawawezi kuvumilia urefu huo. Mara nyingi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akirefusha, bali amehimiza kufanya wepesi. Mmesikia yale aliyomwambia Mu´aadh. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivyo mara moja tu kwa sababu maalum. Hali za watu zinapaswa kuzingatiwa, kama vile udhaifu wa imani na uvumilivu.

Swali:

“… alikuwa akituamuru kufanya wepesi, lakini yeye mwenyewe alituswalisha asw-Swaffaat?”

Jibu: Swalah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa kufanya wepesi. Huu ndio msingi wa kuiga. Alitufundisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufanya wepesi katika swalah. Kumuiga yeye ndio kufanya wepesi. Hata hivyo ikiwa imamu atazingatia hali za watu, kama alivyoamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi ni vyema zaidi kuzingatia hali zao na kutowatia katika majaribio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24904/حكم-اطالة-الامام-القراءة-في-صلاة-الجماعة
  • Imechapishwa: 07/01/2025