Mgonjwa anatakiwa kuswali kiasi cha hali na uwezo wake

Swali: Baba yangu amelazwa hospitali karibu miaka miwili sasa na wala hawezi hata kutikisika na kutawadha. Tunapomwambia kuwa ni wakati wa swalah anaelewa tunachokisema lakini hata hivyo hatawadhi na badala yake anaswali ilihali yuko kwenye kitanda chake.

Jibu: Ndio, anatakiwa kuswali kwa kiasi cha hali yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mgonjwa anaswali kwa kuketi, asipoweza, basi aswali kwa kukaa, asipoweza, basi aswali kwa kulalia ubavu, asipoweza, basi aswali kwa kulala na huku ameielekeza miguu yake Qiblah.”

Mgonjwa anatakiwa kuswali kwa kiasi cha hali yake.

Lakini ikiwa hawezi kutumia maji – kama anavosema muulizaji – basi aletewe udongo msafi. Afanye Tayammum kwa udongo huo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 01/12/2017