Swali: Mgonjwa siku nne kabla ya kufariki aliacha swalah kwa sababu ya kutoweza kutikisika na kutoweza kutawadha. Je, alipiwe swalah?
Jibu: Mgonjwa halipiwi swalah anapoaga dunia. Wagonjwa wengi wanasumbuliwa na jambo hili. Utawaona wanaacha kuswali kwa sababu wamechoka sana, kwa sababu hawana maji ya kutosha ya kutawadhia, udongo wa kuyanyia Tayammum au kwa sababu mavazi yake yana najisi. Matokeo yake wanajitolea fatwa ya kwamba hawahitaji kuswali na kwamba wataanza kuswali tena baada ya kupona. Hili ni kosa kubwa. Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali kutokana na hali yake. Kama anaweza kutawadha, basi atatawadha. Asipoweza kutawadha, atafanya Tayammum. Asipoweza hilo pia, basi ataswali vile alivyo.
Aidha anatakiwa kuswali mavazi yake yakiwa masafi. Asipoweza basi ataswali vile alivyo hata kama mavazi yake yatakuwa najisi.
Vivyo hivyo kuhusu godoro. Ni lazima liwe safi. Lisipoweza kusafishwa au kubadilishwa kwa godoro jengine au kulifunika kwa kitu, basi ataswali vile lilivyo hata kama ni najisi.
Vivyo hivyo kuhusu kueleka Qiblah. Analazimika kuelekea Qiblah. Asipoweza kuelekea Qiblah, basi ataswali kulingana na hali yake.
Muhimu ni kwamba uwajibu wa swalah uko palepale muda wa kuwa bado yuko na akili. Ataswali vile anavyoweza. Hata kama tutakadiria kuwa hawezi kutikisika si kwa kichwa chake wala macho yake, ataswali kwa moyo wake. Baadhi ya watu wasiokuwa na elimu wanaswali kwa kidole. Jambo hili halina msingi katika Sunnah wala katika maneno ya wanazuoni. Kwa hiyo ni lazima kwa mgonjwa kuswali kulingana na hali yake, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[2]
[1] 64:16
[2] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/98-99)
- Imechapishwa: 04/05/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/98-99)
Imechapishwa: 04/05/2026
https://firqatunnajia.com/mgonjwa-ameacha-kuswali/