4 – Kuosha miguu hadi vifundo viwili. Vifundo viwili vinaingia katika maosho. Kila mguu mmoja una vifundo viwili. Vifundo si vile vinavyochomoza juu ya mguu, kama wanavyodhani baadhi ya madhehebu potofu wanaopaka badala ya kuosha ilihali wajibu ni kuosha kwa mujibu wa dalili ya kisomo:

وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

”… miguu yenu hadi vifundoni… ”

Isitoshe Sunnah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia zimebainisha sifa ya wudhuu´ kutokana na hilo. Kuhusu kisomo:

وَأَرْجُلَكُمْ

”… na miguu yenu… ”

kinafasiriwa kuosha kwa upole ili kukusanya baina ya visomo vyote viwili. Kuacha kuosha miguu kwa kujengea juu ya kisomo kinachoashiria kuwa miguu inapaswa kuoshwa na pia jambo hilo likafahamishwa na Sunnah ni katika kufuata maandiko yasiyo wazi na kuacha maandiko yaliyo wazi. Inatosha kama dalili ya upotofu wa waliopotea kuhusu suala la kuosha miguu na kutosheka na kupaka miguu pekee ya kwamba wamejinyima alama ya kung’aa iliyosmewa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika ummah wangu wataitwa siku ya Qiyaamah wakiwa na nyuso na miguu inayoangaza kutokana na athari ya wudhuu´.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah.

Jengine ni kwamba wamejiweka katika matishio ya adhabu yaliyokuja katika maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ole wa visigino vya miguu kutokana na Moto.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 04/05/2026