Swali: Ni ipi hukumu ya muadhini kusema:
حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ
“Njooni katika mafanikio.”
kabla ya kusema:
حَيَّ عَلى الصلاةِ
“Njooni katika swalah.”?
Jibu: Katika hali hiyo anawajibika kurudia kusema:
حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ
“Njooni katika mafanikio.”
baada ya kusema:
حَيَّ عَلى الصلاةِ
“Njooni katika swalah.”
Ni sharti katika adhaana kupangilia jumla. Adhaana imepokelewa namna hii. Yule anayetoa adhaana kwa kutopangilia basi amefanya kitendo kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]
[1] Muslim (1718).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/174-175)
- Imechapishwa: 04/05/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya muadhini kusema:
حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ
“Njooni katika mafanikio.”
kabla ya kusema:
حَيَّ عَلى الصلاةِ
“Njooni katika swalah.”?
Jibu: Katika hali hiyo anawajibika kurudia kusema:
حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ
“Njooni katika mafanikio.”
baada ya kusema:
حَيَّ عَلى الصلاةِ
“Njooni katika swalah.”
Ni sharti katika adhaana kupangilia jumla. Adhaana imepokelewa namna hii. Yule anayetoa adhaana kwa kutopangilia basi amefanya kitendo kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]
[1] Muslim (1718).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/174-175)
Imechapishwa: 04/05/2026
https://firqatunnajia.com/kutoa-adhaana-kwa-kutopangilia-maneno-yake/