Mgonjwa ambaye daktari amemkataza kusujudu

Swali: Baadhi ya wagonjwa wakifanyiwa upasuaji katika jicho moja na daktari akamkatalia kusujudu wanaonekana baadhi yao wakiswali kwa kuketi chini na pengine wakafanya Tayammum.

Jibu: Asujudu kwa kuashiria. Kama amekataliwa kusujudu ainamishe kichwa chake zaidi kuliko Rukuu´ na asifanye Sujuud. Ikiwa yuko na kitambaa kichwani akipanguse. Aoshe uso wake na apanguse kichwa chake.

Swali: Lakini anaswali kwa kuketi chini?

Jibu: Hapana, haijuzu. Ni lazima kusimama isipokuwa ikiwa ni mgonjwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23582/حكم-المريض-الذي-منعه-الطبيب-من-السجود
  • Imechapishwa: 16/02/2024