Kuoanisha kati ya Hadiyth ya kadi na Shahaadah

Swali: Mfano wa Hadiyth ya kadi?

Jibu: Vivyo hivyo kuhusu Hadiyth ya kadi na nyenginezo. Akilazimiana na haki ya shahaadah mbili. Lakini akishuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, akaacha swalah au akakanusha uwajibu wake, ni kafiri. Au akapinga uwajibu wa swawm, uwajibu wa zakaah, uwajibu wa hajj, akazini, akanywa pombe atawajibishwa. Kwa hivyo ni lazima alazimiana na haki ya ´laa ilaaha illa Allaah` na haki ya shahaadah mbili kwa njia ya kutekeleza faradhi za Allaah na kuacha maharamisho Yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23581/الجمع-بين-من-شهد-ان-لا-اله-الا-الله-وحديث-البطاقة
  • Imechapishwa: 16/02/2024