Ni wajibu kwa mgeni anapofika kwa mwenyeji wake na akataka kuswali Sunnah amuulize Qiblah kilipo. Akimwambia kilipo akielekee. Baadhi ya watu wanaona hayaa na hapa haya sio mahali pake. Kuuliza Qiblah kilipo ni hayaa isiyokuwa mahali pake. Baadhi ya watu wanaona hayaa kuuliza Qiblah kilipo ili watu wasisemi ya kuwa hajui. Haidhuru kitu. Aseme anachotaka. Linalompasa ni yeye aulize mahali Qiblah kilipo ili mwenyeji akueleze. Kuna watu wanaona hayaa na hilo linampelekea kujitahidi mwenyewe kuelekea upande fulani na [baadaye] inambainikia kuwa alielekea makosa, katika hali hii ni wajibu kwake kurudi swalah yake kwa sababu ameegemea katika jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/376)
- Imechapishwa: 23/05/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Unapoweza kuuliza Qiblah kisha ukafanya uzembe
Swali: Akikosea Qiblah ndani ya mji? Jibu: Hapana, si sawa. Atakuwa ni mzembe katika mji. Anatakiwa kuilipa, kwa sababu ndani ya mji anaweza kuuliza. Kuna watu anaoweza kuwauliza kilipo Qiblah. Pia kuna misikiti.
In "Qiblah"
Amebahatisha Qiblah kisha imembainikia amekosea
Kuhusu asiyejua Qiblah kilipo, ni wajibu kwake kuelekea Qiblah. Lakini akijitahidi na kufanya bidii kisha baadaye ikambainikia amekosea baada ya kujitahidi, sio wajibu kurudi kuswali tena. Hatusemi kuwa kuelekea Qiblah kwa haki yake kunaanguka. Ni lazima kwake kuelekea Qiblah na ajitahidi kiasi na anavyoweza. Akijitahidi kiasi na anavyoweza kisha ikambainikia…
In "Qiblah"
05. Amebainikiwa kuwa ameswali kinyume na Qiblah
Swali 05: Ni ipi hukumu ikibainika kuwa swalah imeswaliwa kinyume na Qiblah baada ya kujitahidi? Je, kuna tofauti ikiwa hayo yametokea katika nchi ambayo sio ya waislamu, nchi ya makafiri au ikawa mwituni? Jibu: Muislamu akiwa safarini au katika mji ambao asimpate ambaye atamwelekeza katika Qiblah, basi swalah yake ni…
In "1. Sharti za swalah"