Swali: Ni ipi hukumu ya kuogelea na kupiga mbizi?

Jibu: Kinachozingatiwa ni kwamba kusiingie kitu tumboni mwake. Ikiwa anaogelea baharini, ikiwa maji ni ya chumvi basi pengine yakapenyeza. Sisi tumeogelea ndani yake. Wakati mwingine mtu hahisi na tahamaki yamekwishapenyeza kooni. Kwa ajili hiyo tunashauri kujiepusha na jambo hilo. Lakini ikiwa maji si ya chumvi hayapenyezi kooni lakini kuna uwezekano nayo yakafanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 80
  • Imechapishwa: 18/03/2024