Mfanya matabano anaandika Aayah za Qur-aan kwa kuzipindua juu na chini

Swali: Wakati mtu anapoumwa, basi watu wanampeleka kwa baadhi ya watu ambao wanatambulika kwenye midomo ya wajinga kwamba huwakusanya na kuwatenganisha majini. Watu hawa huandika Aayah za Qur-aan kwenye makaratasi. Wakati mwingine Aayah hizi zinakuwa zimepinduliwa chini na juu. Mgonjwa anapewa karatasi hiyo na kuambiwa kuwa asiifungue na kwamba aiweke mahali maalum. Mara nyingine wanaandika fumula zisizojulikana kwenye sinia na wanamwamrisha yule mgonjwa azioshe kwa maji mpaka upotee ule wino. Baada ya hapo mgonjwa yule anakunywa maji yale. Je, inafaa kwenda kwa watu kama hawa?

Jibu: Ni haramu kwenda kwa watu kama hawa wanaondika fomula zisizotambulika. Kwa sababu hatujui ni kipi wanachoandika. Kile kitendo cha wao kuandika Aayah za Qur-aan zilizopinduliwa juu na chini inafahamisha kwamba wanashirikiana na ambao wanawatumikia na wanawaamrisha waziandike Aayah za Qur-aan kwa njia ya kupindua chini na juu. Ikiwa wanazuoni wametofautiana kama inafaa kuandika Qur-aan kwa hati isiyokuwa ya msahafu wa ´Uthmaan, tusemeje juu ya yule ambaye anaandika Aayah za Qur-aan kwa kuzipindua juu na chini?

Nawanasihi watu hawa na wengineo ambao wanawapoteza watu kutokamana na mfumo huu uliopinda. Tubuni kwa Allaah kabla ya kujiliwa na adhabu kisha msinusuriwe. Rejeeni katika Qur-aan na Sunnah. Ikiwa mnataka kuwanufaisha waja wa Allaah basi iwe kwa njia inayokubalika katika Shari´ah na sio kwa njia iliyoharamishwa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/57-58)
  • Imechapishwa: 01/07/2026