Swali: Ni jambo limeenea katika baadhi vijiji yale yanayoitwa matabano ya nge. Inakuwa namna hii msomaji analeta mafuta na sukari anavyochanganya kisha baadaye anasoma juu yake dhidi ya nyota. Kisha mfanya matabano anamwamrisha yule anayemfanyia matabano anywe ule mchanganyiko na asimweleze yeyote kuhusu matabano hayo. Aidha yule anayefanyiwa matabano anaambiwa kuwa hana ruhusa ya kuwaua unge atakayewaona na hivyo ndivo anavyokingwa na kuchomwa na nge. Matabano haya bei yake ni pesa 1. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Matabano haya dhidi ya kudonolewa na nge ni matabano ya kizushi yasiyokuwa na msingi wowote, si inapokuja katika upande wa dini wala sayansi ya tiba. Ni aina fulani ya shirki, kwa sababu sio haina mashiko upande wa dini wala kihisia. Bali ni mawazo tu.

Sababu nyingine ni kwamba matabano hayo yanapingana na Sunnah ambayo imeamrisha kuwaua nge. Mtu ameamrishwa kuwaua nge ijapokuwa amewaona wakati yuko anaswali, watakuwa Makkah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanyama watano wote ni wenye madhara na wanauliwa katika maeneo halali na maeneo haramu: kunguru, kite, nge, panya na mbwa menye kuuma.”[1]

Vilevile Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha:

“Kuwaua weusi wawili ndani ya swalah: nge na nyoka.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1829) na Muslim (1198).

[2] Ahmad (2/233), Abu Daawuud (921), at-Tirmidhiy (390), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh, an-Nasaa’iy (1203) na Ibn Maajah (1245).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/58-59)
  • Imechapishwa: 29/06/2026