Anaswali Fajr pale wakati anapoamka kwenda kazini

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anaswali Fajr pale ambapo umefika wakati wa kwenda kazini? Anapoambiwa kuwa kitendo hicho hakijuzu, anatumia hoja kwa kusema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu watatu; aliyelala hadi aamke, mdogo hadi awe mkubwa na mwendawazimu hadi apate fahamu.”[1]

Jibu: Nini anachosema bwana huyu endapo kazi yake inaanza nusu saa baada ya kuchomoza kwa jua? Ataamka au atajenga hiyohiyo? Ataamka. Ikiwa unaamka kwa ajili ya jambo la kidunia, ni kwa nini basi huamki kwa ajili ya jambo la Aakhirah? Isitoshe Hadiyth inamuhusu yule mtu ambaye amepitiwa na usingizi au hana wa kumwamsha. Kuhusu mtu ambaye anaweza kuamka kwa njia moja au nyingine si mwenye kupewa udhuru. Ni wajibu kwa mtu huyu atubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) na afanye bidii kuamka na kuswali pamoja na waislamu wenzake.

[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/23)
  • Imechapishwa: 29/06/2026