84. Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim kuhusu Pepo itayoteketea

Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahumaa Allaah) wamenasibishiwa maoni yanayosema kuwa Moto utateketea. Kama manasibisho hayo yamesihi basi wanakusudia ile ngazi waliopo watenda madhambi wapwekeshaji. Hiyo itamalizika na hakuna yeyote atakayebaki humo kabisa. Utafika wakati milango yake ifunguliwe na kusibaki humo yeyote. Kwa hiyo kunaposemwa kuwa ipo siku Moto utateketea, kunakusudiwa ile ngazi ya watenda madhambi wapwekeshaji – na sio zile ngazi walizoumbiwa makafiri, wanafiki na wapagani, kama kinavyotamka wazi Kitabu cha Allaah kinachobainisha na akatamka wazi Mtume wa Allaah, mkweli, mwenye kusadikishwa na mwenye kuaminiwa, Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mpaka hapa ndio mwisho wa maelezo yangu juu ya kitabu hichi kwa jina “at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah”. Mwishoni namuomba Allaah atufahamishe dini ili tuweze kuijua na kuifanyia kazi mpaka pale tutapofishwa na Mola wetu. Swalah, amani na baraka zimwendee Mtume wetu na mbora wa watu Muhammad, watu wa nyumbani kwake, Maswahabah zake wa kale na bora na wale wote wema na watukufu watakaowafata.

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 178
  • Imechapishwa: 29/06/2026