Washirikina wa shirki kubwa, makafiri wa ukafiri mkubwa, wanafiki wa unafiki mkubwa na wapaganaji ndio ambao watakaa Motoni milele na hawatokufa wala kupata uhai:
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا
”Hakika wale waliokanusha Aayah Zetu, Tutawaingiza Motoni. Kila ngozi zao zitakapobanikika zikachoma Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje vyema adhabu. Hakika Allaah daima ni Mwenye nguvu aliyeshinda, Mwenye hekima wa yote.”[1]
وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ
”Wale waliokufuru watapata moto wa Jahannam – hawatahukumiwa wakafa na wala hawatakhafifishiwa adhabu yake. Namna hiyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwingi wa kukufuru. Nao watapiga mayowe humo “Mola wetu! Tutoe tutende mema yasiyo yale tuliokuwa tukitenda.” [Wataambiwa] “Je, kwani hatukukupeni umri wa kukumbuka mwenye kukumbuka humo na alikujieni mwonyaji. Basi onjeni! Kwani madhalimu hawana yeyote yule wa kuwanusuru.”[2]
وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا
“… wala kuwaongoza njia; isipokuwa njia ya Jahannam wadumishwe humo milele.”[3]
لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا
”Watabakia humo karne baada ya karne.”[4]
Bi maana milele. Kwa sababu Aakhirah ndio makazi yenye mwanzo lakini hayana mwisho. Wakazi wa Motoni watakaa Motoni milele ambapo hawakufa ndani yake wala kupata uhai. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema kuhusu waliokula khasara:
لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
“… hatouingia kuchomeka isipokuwa muovu mkubwa, ambaye amekadhibisha na akakengeukia mbali.”[5]
Vivyo hivyo kuhusu ambaye ataingia Peponi; hatotoka humo hata siku moja. Pepo haiteketei na wala haiishi. Pepo haina mwisho, ndivo inavyofahamisha Qur-aan na Sunnah. Wale watu ambao wamechezewa na shaytwaan, wakaongozwa na akili zao na kupinda kutokana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah pale waliposema eti ipo siku Pepo na Moto vitateketea na kumalizika.
[1] 4:56
[2] 35:36-37
[3] 4:169
[4] 78:23
[5] 92:15-16
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 177-178
- Imechapishwa: 29/06/2026

Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 177-178
Imechapishwa: 29/06/2026
https://firqatunnajia.com/83-pepo-ya-milele-moto-wa-milele/