Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Swalah ya jeneza anaswaliwa muislamu aliyekuwa akimpwekesha Allaah. Huyu anaombewa msamaha. Hatakiwi kunyimwa hilo. Wala haitakiwi kuacha kumswalia kutokana na dhambi aliyotenda, sawa iwe kubwa au ndogo. Jambo lake liko kwa Allaah (Ta´ala).
MAELEZO
Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba wanawaswalia swalah ya jeneza wapwekeshaji, muda wa kuwa sio makafiri, washirikina, unafiki wa kiitikadi. Wakati wapwekeshaji watenda madhambi wanapokufa ni lazima kuwaandaa kwa kuwaosha miili yao, kuwavika sanda, kuwazika, kuwaswalia swalah ya jeneza na kuwaombea du´aa. Haijalishi kitu hapa hata kama ni mtenda madhambi makubwa. Wanamuombea du´aa na wanachelea juu yake, kwa sababu amekufa bila ya kutubia. Hata hivyo wanathibitisha kuwa mafikio ya mwisho ya kila mpwekeshaji ni Peponi ijapo anaweza kukaa Motoni kwa kipindi kirefu au akaadhibiwa ndani ya kaburi. Mafikio yake ya mwisho ni Peponi kutokana na fadhilah za Allaah kisha uombezi wa waombezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Allaah (´Azza wa Jall) atasema siku ya Qiyaamah:
“Mtoeni Motoni yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na dinari, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na nusu dinari, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na kokwa ya tende, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na dudu mchungu na halafu yule ambaye yuko na imani ya chini chini chini kabisa kuliko dudu mchugu.”[1]
Kwa maana nyingine hakuna mpwekeshaji yeyote ambaye atakaa Motoni milele.
[1] al-Bukhaariy (7510) na Muslim (193).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 175
- Imechapishwa: 29/06/2026
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Swalah ya jeneza anaswaliwa muislamu aliyekuwa akimpwekesha Allaah. Huyu anaombewa msamaha. Hatakiwi kunyimwa hilo. Wala haitakiwi kuacha kumswalia kutokana na dhambi aliyotenda, sawa iwe kubwa au ndogo. Jambo lake liko kwa Allaah (Ta´ala).
MAELEZO
Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba wanawaswalia swalah ya jeneza wapwekeshaji, muda wa kuwa sio makafiri, washirikina, unafiki wa kiitikadi. Wakati wapwekeshaji watenda madhambi wanapokufa ni lazima kuwaandaa kwa kuwaosha miili yao, kuwavika sanda, kuwazika, kuwaswalia swalah ya jeneza na kuwaombea du´aa. Haijalishi kitu hapa hata kama ni mtenda madhambi makubwa. Wanamuombea du´aa na wanachelea juu yake, kwa sababu amekufa bila ya kutubia. Hata hivyo wanathibitisha kuwa mafikio ya mwisho ya kila mpwekeshaji ni Peponi ijapo anaweza kukaa Motoni kwa kipindi kirefu au akaadhibiwa ndani ya kaburi. Mafikio yake ya mwisho ni Peponi kutokana na fadhilah za Allaah kisha uombezi wa waombezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Allaah (´Azza wa Jall) atasema siku ya Qiyaamah:
“Mtoeni Motoni yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na dinari, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na nusu dinari, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na kokwa ya tende, kisha yule ambaye moyoni mwake kuna imani sawa na dudu mchungu na halafu yule ambaye yuko na imani ya chini chini chini kabisa kuliko dudu mchugu.”[1]
Kwa maana nyingine hakuna mpwekeshaji yeyote ambaye atakaa Motoni milele.
[1] al-Bukhaariy (7510) na Muslim (193).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 175
Imechapishwa: 29/06/2026
https://firqatunnajia.com/82-kuwaswalia-waislamu-wote-wanaokufa-swalah-ya-jeneza/