Muda baina ya kuadhiniwa na kukimiwa

Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitenga muda maaluma baina ya kuadhiniwa na kukimiwa?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali pale tu unapoingia wakati wa swalah isipokuwa ´Ishaa. Hakika alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisubiri watu; akiwaona wamehudhuria basi huswali, na akiwaona wamechelewa anachelewesha[1]. Alikuwa akisubiri nyumbani mpaka anakuja muadhini kumweleza aje kuswali. Mwingine anatoka nje mwenyewe bila ya kujuzwa na muadhini.

Kwa hiyo Sunnah ni kuharakisha swalah zote isipokuwa ´Ishaa. Dhuhr pia inabaguliwa wakati wa joto kali. Zile swalah ambazo zina Rawaatib, kama vile Fajr na Dhuhr, watu wanatakiwa kupewa wakati wa kutosha wa kuweza kutawadha na kuziswali swalah hizi baada ya adhaana.

[1] al-Bukhaariy.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/190-191)
  • Imechapishwa: 01/07/2026