Swali: Imeenea katika njia za mawasiliano mtu ambaye amemuota Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amempa wasia na akamuahidi furaha endapo ataeneza wasia huu na huzuni na majuto endapo hatofanya hivo.

Jibu: Ni shaytwaan. Sio kila anayemuota Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuona kweli. Yule mtu ambaye anazijua sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye anaweza kumuona. Shaytwaan hawezi kujifananisha na umbile lake ya kihakika. Mtu ambaye hazijui sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asiaminiwe. Kuna uwezekano ikawa ni shaytwaan.

Jengine ni kwamba wasia na maamrisho yamekatika kwa kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna maamrisho, wasia wala na mambo ya Shari´ah baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yale ambayo Allaah ametuwekea katika Shari´ah yanatosheleza. Shari´ah ya Kiislamu inatutosheleza. Hatutaki kuwa na ziada, maamrisho, mahamasisho ya kueneza na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ayatquran-26-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020