Swali: Je, anawajibika wakati mchungaji anapochinja bila ya idhini ya mmiliki?
Jibu: Hawajibiki. Akiwa ni mwenye kufanya vyema analipwa thawabu na anashukuriwa. Akichelea juu ya mnyama kufa au kuchukuliwa na mbwa mwitu na hivyo akamchukua na kumchinja, anashukuriwa na kulipwa thawabu. Anastahiki kushukuriwa.
Swali: Akimchinja na asitikisike na isitoke damu?
Jibu: Udhahiri wa maneno ya wanazuoni ni kwamba ni lazima atikisike. Vinginevyo ameshakufa kwa mujibu wa maneno ya baadhi ya wanazuoni. Hayo ndio maoni ya Taqiyy-ud-Diyn Ibn Taymiyyah. Hata hivyo yanatakiwa kukaguliwa vyema. Baadhi ya Salaf wanaona kuwa ni lazima atikisike na kuhakikishwe kuwa yuko hai.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24010/حكم-الراعي-اذا-ذبح-دون-اذن-المالك
- Imechapishwa: 17/08/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket