Kukata kichwa wakati wa kumchinja mnyama

Swali: Uhalisia ni kwamba wengi ambao wanachinja hawakati shingo. Hata hivyo wanapochinja kisu kinaingia kwenye uboho na hivyo kuukata bila ya kuvunja.

Jibu: Udhahiri ni kwamba inatakiwa kuacha hayo yote na kwamba inatosha tu kukata koo, umio na mishipa ya pumzi. Asivunje kichwa. Lakini hata hivyo akikata kichwa mara moja inasihi, kwa sababu lengo litakuwa limefikiwa. Hata hivyo bora ni kuacha kufanya hivo kutokana na yale yaliyopokelewa kutoka kwa ´Umar, Ibn ´Umar na Sayyid bin Musayyab kwa cheni ambayo anakosekana swahabah ndani yake. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24014/حكم-كسر-الراس-في-ذبح-الانعام
  • Imechapishwa: 17/08/2024