Swali: Katika kijiji chetu kuna bwana mmoja mlevi na wala haswali anayekuja katika darsa yangu nyumbani baada ya Fajr kusikiliza. Unatunasihi nini na tumwache aje kusikiliza darsa?

Jibu: Mwache ahudhurie. Hata hivyo mnasihi baina yako wewe na yeye. Mweleze kuwa unamuona ni mwenye kupenda kheri, anakuja katika darsa, kwamba yeye ni bora kuliko anavyoonekana na kwamba analazimika kutubia kwa Allaah. Pengine Allaah akamuokoa kwa sababu yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 17/08/2024