Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا

“Hakika si venginevyo waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zaozinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea; ambao wanasimamisha swalah na hutoa sehemu katika yale tuliyowaruzuku – hao ndio waumini wa kweli!” (08:02-04)

Bi maana kunapotajwa ukubwa, utukufu na ufalme Wake, basi mioyo yao inaingiwa na khofu na hutetemeka. Mtu anaathirika. Baadhi ya Salaf walikuwa wanaposomewa baadhi ya Aayah za khofu wanapatwa na ugonjwa mpaka wanakuja watu kuwatembelea. Lakini sisi mioyo yetu ni migumu. Tunamuomba Allaah ailainishe mioyo yetu. Tunasomewa Aayah za khofu na zinapita lakini ni kana kwamba si lolote na si chochote. Tunamuomba Allaah usalama.

Muumini ni yule ambaye anapotajwa Allaah moyo wake unatikisika na anaogopa.

Kuna Salaf ambao pindi walipokuwa wanaambiwa “Mche Allaah!” wanatetemeka mpaka kinaanguka kitu alichokishika mkononi mwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/544)
  • Imechapishwa: 10/07/2023