Swali: Kutoa mawaidha kwenye harusi na kilioni ni jambo limekatazwa na ni Bid´ah?

Jibu: Ni sawa. Ni jambo zuri. Kupeana mawaidha na nasaha mahala ambapo watu wamekusanyika, sawa ikiwa watakusanyika harusini au kwa jambo miongoni mwa mambo, akatumia fursa hii na kuwakumbusha, hili ni jambo zuri. Hakuna yeyote aliyesema kuwa ni Bid´ah.

Lakini ikiwa mkutano huu ni wa Bid´ah, kama mkutano wa maombolezo [ya siku tatu n.k.], hili halijuzu. Usije na wewe ukawasaidia kwa hilo. Ama mkutano ikiwa ni wenye kuruhusiwa au ni mkusanyiko wa ´ibaadah Msikitini au kusoma, kupeana mawaidha ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-30.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020