[Walinganizi] tunatakiwa kuwa na subira kutokana na yale tunayosikia na kuambiwa watu wanayosema kuhusu sisi kwa sababu ya kulingania katika dini ya Allaah. Tunatakiwa kuona haya kama ni kupandishwa daraja na sababu ya kusamehewa madhambi yetu. Pengine Da´wah yetu ikawa na kasoro; upungufu wa Ikhlaasw au namna ya jinsi tunavolingania na njia tunazotumia. Maudhi haya tunayosikia ikawa ni kafara ya mapungufu yetu. Haijalishi kitu mtu kiasi na atakavyofanya bado mapungufu yatapatikana. Hawezi akafanya kitendo kikamilifu kwa hali yoyote ile isipokuwa akitaka Allaah. Hivyo basi, mtu akipatwa na maudhi kwa sababu ya kulingania katika dini ya Allaah, hili ni kwa njia ya kukamilisha Da´wah yake na kunyanyuliwa daraja zaidi. Kwa hivyo awe na subira na wakati huo huo akitarajia malipo kutoka kwa Allaah. Asirudi nyuma. Asilalamike. Anachotakiwa ni kuwa na subira. Dunia sio ndefu. Ni masiku machache kisha inaisha. Hivyo kuwa na subira mpaka Allaah alete Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/241-242)
  • Imechapishwa: 06/03/2023